See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

ZAMA ZA UONGOFU


 KHULAFA


Hakika zama za Makhalifa waongofu zime ungana na zama za utume, kumetimia katika zama hizo bishara zilizo tajwa katika Qur'ani na Sunnah, mfano wa neno lake Allah ﷻ alietukuka;وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ

 

[Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.]   [Suratun Nur-55]. 

Na akasema Allah Alie tukuka;

{وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ}

 

[Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi.]   [Suratul Qasas -5] 

Alikuwa Mtume akiwabashiria Masahaba zake akisema;

[والله ليتمن هذا الأمر حتى يسير الراكب من صنعاء إلى حضرموت، لا يخاف إلا الله]

 


[Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu Atalitimiza jambo hili (Uislamu) mpaka aende msafiri juu la kipando kutoka San'aa kwenda Hadhramaut haogopi ila Allah] 

[Imepokelewana Bukhari - Fathul Sari; 7/195 na Ahmad katika Musanad yake; juzu ya 5/110) 

Amemuelezea Mtume  Suraqa ibn Malik kuwa atakivaa vikuku vya mfalme; wa Kisra [AI Isaba 2/89]. 
Na katika kuchimba handaki kabla ya vita vya Ahzab, lilikingama kwa baadhi ya masahaba jiwe akainuka Mtume ili alivunje,na wakati alipolipiga jiwe lile lilitoka cheche, na akapiga "takbira", na wakapiga waislamu "takbira" pamoja nae, kisha akalipiga mara ya pili likatoa cheche, akapiga "takbira", na wakapiga waislamu "takbira" pamoja nae, kisha akalipiga kwa mara ya tatu, akapiga "takbira", na wakapiga waislamu "takbira" pamoja nae, akasema mwisho wapigo la kwanza Allah ﷻ ni mkubwa nimepeWa funguo za Sham. Na apa kwa Allah ﷻ hakika yangu mimi naona majumba yake mekundu hivi sasa, kisha alipopiga mara ya pili akasema, 'Allahu Akbar' nimepewa funguo za Faris. Naapa kwa Allah ﷻ naona jumba leupe la Madaain kisha alipolipiga mara ya tatu alisema; 'Allahu Akbar' nimepewa funguo za Yemen. Hivi sasa hapa nilipo nayaona milango ya San'aa]  [Al-Futuh al Islamiyyah, P21. Musnad Ahmad 4:303].

Mwenyezi Mungu alotukuka na sifa mbaya aliwafanya Masahaba kuwa ni makhalifa katika ardhi, akawasimamishia Dini yao, akawafanya viongozi na akawafanya mawarithi. Waliigia Yemen, Sham na Faris hali ya kuikomboa (futahi) miji hivo na kunusurika; Na hakika lilitimia jambo hllo mpaka akaenda msafiri kutoka San'aa kwenda Hadhramaut hali ya kuwe na amani na utunvu. 

zama za Uongofu wa Makhalifa ambazo hazizidi miaka
thelathini, baada ya kufa kwa Mtume nave ndiyo
kutimia kwa zama za utume.*


 * Khulafau Arrashidun 15-18

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it./Thumbr.php" data-layout="standard" data-width="100" data-action="like" data-show-faces="false" data-share="false">
// /Thumbr.php'> // /Thumbr.php' action='share'>

logompya


Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

8111967
TodayToday10061
Highest 09-25-2020 : 24573
US
Guests 335

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Masomo

title_5f762854ebb346409165641601579092
title_5f762854ebd1512810949811601579092
title_5f762854ec16d2706064931601579092
 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

title_5f7628551834618853115311601579093
title_5f7628551846520266633401601579093

HUDUMA MPYA

: 2 + 8 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com