See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

SOMO LA FIQHI


maji yakusomewa


Kwanza: Maji Yenye kutwahirisha

1. Maji ya Kawaida:

Nayo ni maji ambayo yamebaki katika sifa yaliyoumbiwa nayo, kama maji yanayoteremka kutoka mawinguni, kama vile mvua, theluji na mvua ya barafu au yenye kutembea ardhini, kama maji ya bahari, mito na maji ya mvua na maji ya visima. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema

 

وَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً طَهُورًا}    الفرقان:48

 

[Na tumeyateremsha kutoka mbinguni maji safi]    [25: 48]

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

 

وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً لِّيُطَهِّرَكُم بِهِ}     الأنفال:11

 

[Na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni ili kukusafisheni kwayo]    [8: 11]

 

Na Mtume alikuwa akiomba na kusema:

 

  اللهم اغسل خطاياي بالماء والثلج]    رواه البخاري ومسلم]

 

[Ewe Mola wangu! Nitakase na makosa yangu kwa theluji, maji na barafu]   [ Imepokewa na Bukhari na Muslim].

Na alisema tena kuhusu maji ya bahari:

 

هُوَ الطَّهُورُ مَاؤُهُ الْحِلُّ مَيْتَتُهُ]    رواه أحمد أبوداود]

 

[Maji yake ni yenye kutwahirisha na mfu wake ni halali]       [Imepokewa na Ahmad na Abu Daud.]

 

2. Maji yaliyotumiwa:

Nayo ni maji yanayotiririka kutoka kwenye viungo vya mwenye kutawadha au mwenye kuoga. Hayo si makosa kuyatumia kujitwahirishia,

 

عن ابن عباس قال اغتسل بعض أزواج النبي صلى الله عليه وسلم في جفنة فأراد رسول الله صلى الله عليه وسلم أن يتوضأ منه فقالت يا رسول الله إني كنت جنبا فقال إن الماء لا يجنب

Kutoka kwa Ibn Abbas Radhi za Allah ziwe juu yake  kuwa alisema kuwa mmoja katika wake wa Mtume alioga kwenye chombo, na Mtume wa Mwenyezi Mungu akataka kutawadha kutoka kwenye chombo hicho. Yule mkewe akasema: «Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi nilikuwa na janaba.” Akasema: [Maji hayaathiriki na Janaba]    [Imepokewa na Tirmidhi.].

 

3. Maji Yaliyochanganyika na kitu Twahara:

Nayo ni maji yaliyochanganyika na kitu twahara kama majani ya mti au mchanga au kutu kwenye matanki ya maji na kisiache athari kwenye yale maji yenye kuyafanya yasiitwe maji ya kawaida. Kwa kauli ya mtume kuwaambia wanawake waliosimama kumshughulikia binti yake aliyekuwa amekufa (Nae ni bi ruqiya Radhi za Allah ziwe juu yake):

 

 اغسلنها ثلاثا أو خمسا أو أكثر من ذلك إن رأيتن ذلك بماء وسدر واجعلن في الآخرة كافورا أو شيئا من كافور]    رواه البخاري ومسلم]

 

[Mwosheni mara tatu au nne au zaidi ya hizo kama itahitajika, kwa maji na majani ya mkunazi, na mwishoni mwake kafuri]      [Imepokewa na Bukhari na Muslim]


logompya


Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

7314857
TodayToday2235
Highest 08-06-2020 : 13052
US
Guests 267

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Masomo

title_5f34f110befdd17543385371597305104
title_5f34f110bf09e18496811611597305104
title_5f34f110bf17d5565172251597305104
 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

title_5f34f110e62b09628573151597305104
title_5f34f110e637d14254764651597305104

HUDUMA MPYA

: 5 + 3 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com