See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


مختوم


Sauti ya ukweli haikuacha kuvuma katika pande zote za Makka, mpaka ilipoteremka kauli ya Mwenyezi Mungu Aliye Mtukufu: {فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ}

 

[Basi (wewe) yatangaze uliyoamrishwa (wafa usijali upinzani wao) na ujitenge Mbali na (Vitendo 'Vya) hao washirikina.]   [15:94] 

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akasimama na kuwaonya dhidi ya mambo ya ovyo ya kishirikina na upuuzi wake. Akawa anawabainishia ubaya wa masanamu na udhaifu wake, akawa akitoa mifano mingi, kuonyesha udhaifu wa hayo masanamu. Akawawekea wazi, kwa kuzitumia dalili zilizowazi, kuwa mwenye kuyaabudu masanamu, na akayafanya kuwa ni kiungo kati yake na Mwenyezi Mungu  kwa hakika mtu huyo atakuwa katika upotevu ulio wazi. 

Watu wa Makka walighadhibishwa, walishangaa na kugutuka wakati waliposikia sauti inayodhihirisha ukweli, kuwakhofisha na upotevu, ushirikina na watu waliokuwa wakiabudu masanamu. Sauti yake ilifanana na sauti ya radi iliyoyavunja mawingu, ikatoa mweko na kulitetemesha anga lililokuwa tulivu. 

Makuraishi walisimama na kujiandaa kuyazima mageuzi na mapinduzi haya yaliyochomoza ghafla, kwa vile walipata khofu kuwa mageuzi haya yangeondosha mambo yao ya kuiga na yale ambayo waliyarithi. 

Makuraishi walisimama imara katika msimamo wao kwa sababu waliamini kuwa maana ya kuamini ni kuukanusha Uungu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu , na maana ya kuuamini Utume na siku ya mwisho ni kujisalimisha kikamilifu na kutegemeza mambo yote moja kwa moja kwa Mwenyewe Mwenyezi Mungu na kuwa haingebaki kwao khiyari (uhuru) katika nafsi zao au mali zao, sembuse kwa watu wengine.


bibaner


Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

4726478
TodayToday3404
Highest 10-31-2019 : 7656
US
Guests 113

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Makkah

title_5dcd5f0c6adcf1791660861573740300  
title_5dcd5f0c6aec13951458011573740300  
title_5dcd5f0c6afd620708826401573740300  

 

 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

 
title_5dcd5f0c8d62e6414565231573740300

HUDUMA MPYA

: 13 + 14 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com